Tunakaribisha shirika lako kuwasilisha uteuzi kwa Awamu ya 2025 (Mwaka wa 22) Tuzo za Kimataifa za Biashara (International Business Awards®), tuzo kubwa zaidi za biashara ulimwenguni.
Ikiwa ungependa kupokea zana ya kuingia, ikiwa na maagizo kamili kuhusu jinsi ya kuandaa na kuwasiisha uteuzi wako, wasilisha anwani yako ya barua pepe hapa na tutakutumia barua pepe. Tuna sera kali ya faragha na hatutashiriki anwani yako ya barua pepe kwa mtu mwingine yeyote, kwa sababu yeyote.
Kiswahili
Huu ndiyo ukurasa pekee kwenye tovuti hii ambao utaona katika lugha hii. Kurasa zingine zote ziko katika Kiingereza, kama vile zana ya kuingia. Hii ni kwa sababu tunahitaji kuwa uteuzi uwe umewasilishwa kwa Kiingereza, ili wataalamu wa biashara duniani kote waweze kushiriki katika mchakato wa kuhukumu Ifuatayo ni muhtasari mfupi wa IBAs, mahitaji ya uwasilishaji, na manufaa ya kushiriki. Ikiwa utaamua kuwa shirika lako litawasilisha uteuzi kwa IBAs, kumbuka kwamba uteuzi wako lazima uwe umeundwa kwa kiingereza.
Tuzo za kimataifa za biashara ni mpango tu wa tuzo wa kimataifa ili kutambua mafanikio katika kila sehemu ya mahali pa kazi. Shirika la Tuzo la stevie, ambalo linapeana tuzo, liko Marekani. Wao ni waandaaji wa mashindano tofauti tofauti ya Tuzo za Stevie, ambayo unaweza kujifunza kuhusu www.StevieAwards.com. Nyara ya Tuzo za Stevie imekuwa mojawapo ya tuzo kubwa zaidi duniani inayotamaniwa.
Katika mwaka wa 2024, Stevie Awards za Kimataifa (International Stevie Awards) zilikabidhiwa mashirika na watu kutoka mataifa zaidi ya 60. Bonyeza hapa kuona orodha ya washindi katika awamu ya 2024.
Kuna aina nyingi za makundi ya tuzo ambapo utachagua kutoka katika Tuzo za Kimataifa za Biashara. Ikiwa utahiari kuhudhuria, utachagua makundi ambayo yanaoana na mafanikio ambayo Shirika lako linataka kutambuliwa kwa, na uandae uteuzi wako kulingana na maelekezo kwa makundi hayo. Miongoni mwa aina ya makundi yanayopatikana ni kama yafuatavyo:
- Tuzo za Kampuni ya Mwaka
- Tuzo za Mahusiano ya Umma
- Tuzo za Huduma kwa Wateja
- Tuzo za Rasilimali za Watu
- Tuzo za Teknolojia ya Habari
- Tuzo za Usimamizi
- Tuzo za Mauzo
- Ain azote za vyombo vya habari, ikiwa ni pamoja na Tuzo za Mtandao, Tuzo za Ripoti ya Mwaka, Tuzo za Tukio, na Tuzo za video
- Tuzo za Utendaji wa Biashara
- Tuzo za Bidhaa Mpya
Orodha na maelezo ya makundi yako katika zana ya kuingia.
Katika kategoria nyingi una chaguo la kuwasilisha video ya hadi dakika tano (5) kukuhusu au mafanikio ya shirika lako katika kategoria zako ulizochagua, au majibu yaliyoandikwa kwa maswali ya kategoria hizo.
Tumekusanya orodha ya sababu 10 ambazo shirika lako linapaswa kuwasilisha uteuzi katika tuzo. Tathmini orodha hapa.
Shirika lolote ulimwenguni linaweza kushiriki. Awamu ya 2025 ya Tuzo za Biashara za Kimataifa (International Business Awards) itatambua mafanikio ya mashirika na watu binafsi kutoka 1 Januari 2023.
Kuna tarehe tatu za makataa kwa usajili. Aprili 9 ni tarehe ya makataa ya mapema, kwa ada ya kuingia iliyopunguzwa. Mei 7 ndio tarehe ya makataa ya mwisho. Usajili uliochelewa utakubaliwa hadi Juni 11 na malipo ya ada ya kuchelewa.
Uteuzi katika makundi mengi unahitaji malipo ya ada ya kuingia, lakini kuna baadhi ya makundi ambayo unaweza kuingia kwa bure. Malipo yoyote ya kuingia yanayohitajika yameorodheshwa katika zana ya kuingia. Malipo yanapaswa kufanywa kwa Dola za Marekani, aidha kwa kadi ya mkopo, hundi inayotolewa kwa benki ya Marekani, au uhamisho wa pesa kati ya benki.
Washindi wa Awamu ya 2025 ya Stevie Awards za Kimataifa (International Stevie Awards) watatangazwa mnamo Agosti 13. Baadaye, vikombe vya Stevie Award na Medali za Fedha na Shaba zitawasilishwa wakati wa sherehe huko Uropa mwezi wa Oktoba.
Tuzo za Kimataifa za Biashara zina wawakilishi katika nchi nyingi. Wawakilishi hawa watasambaza habari na kusaidia mashirika katika nchi kushiriki katika tuzo hizo. Kuamua ikiwa kuna mwakilishi yeyote katika nchi yako, bofya hapa.
Unaweza pia kuwasiliana na waandaaji katika anwani ifuatayo:
The Stevie Awards
10560 Main Street, Suite 519
Fairfax, Virginia 22030, USA
Simu: +1 703-547-8389
Faksi: +1 703-991-2397
Barua pepe: help@stevieawards.com